Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Julai/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Julai/2022

SIKU 22 YA 31

Wakafurahi pamoja naye ... Akaanza kunena akimsifu Mungu (m.58, 64). Neno ”furaha” limetumika mara nyingi katika Injili ya Luka. Tumeshalikuta katika m.14 na 47. Kiini cha furaha ni neema ya Mungu ambalo pia ni jambo tunalolikuta mara nyingi katika injili hii. Kwa mfano, tazama m.30 anaposema, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu. Kwa hiyo ni furaha ya kumfurahia Bwana kutokana na neema aliyotukirimia. Na neema yake hasa ni kumtuma Mwana wake ili atuokoe! Furaha hii ilipobubujika kwa Mariamu na Zakaria wakatamka maneno mazuri sana juu ya Mungu. Wakasema, Kwa kuwa Mwenye nguvu amenitendea makuu, Na jina lake ni takatifu. Na rehema zake hudumu vizazi hata vizazi Kwa hao wanaomcha (m.49-50).

siku 21siku 23

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Julai/2022

Soma Biblia Kila Siku Julai/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Julai pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Zakaria na Luka. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/

Mipango inayo husiana