Soma Biblia Kila Siku Julai/2022Mfano
Si kwa bahati mbaya kwamba Yesu, Mwana wa Mungu, alilazwa katika hori ya kulia ng’ombe, bali ni ishara: Hii ndiyo ishara kwenu; mtamkuta mtoto mchanga amevikwa nguo za kitoto, amelala katika hori ya kulia ng'ombe (m.12). Ulikuwa ni mpango wa Mungu iwe hivyo! Na malaika hawakujifunua kwa viongozi wa dini pale Yerusalemu bali kwa watu wa chini kabisa, yaani, waliochunga mifugo shambani. Na Mwana wa Mungu hakuzaliwa na binti wa mfalme au kaisari bali na binti wa kawaida aliyemcha Mungu (kama Mariamu anavyodokeza katika 1:52 akisema kuhusu Mungu, wanyonge amewakweza). Ili kuelewa vizuri jambo hili la ajabu sikililiza maneno ya ya Paulo, anasema, Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake (2 Kor 8:9).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Julai/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Julai pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Zakaria na Luka. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/