Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Julai/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Julai/2022

SIKU 29 YA 31

Yohana Mbatizaji alikuwa chombo teule cha Mungu cha kuleta uamsho kwa watu wake. Yohana aliwaleta Waisraeli kwa Mungu kwa wingi kuliko manabii wengine waliowahi kuishi katika Israeli. Kwa hiyo walimfananisha na nabii Eliya (Yn 1:21, Wakamwuliza, Ni nini basi? U Eliya wewe?), na Yesu alimpa sifa kwamba yeye ni zaidi ya nabii: Mlitoka kwenda kuona nini? Nabii? Naam, nawaambia, na aliye zaidi ya nabii. Huyo ndiye aliyeandikiwa haya, Tazama, namtuma mjumbe wangu Mbele ya uso wako, Atakayeitengeneza njia yako mbele yako. Nami nawaambia, Katika wale waliozaliwa na wanawake hakuna aliye mkuu kuliko Yohana (7:26-28). Hata hivyo hatuna kitabu chake kama cha manabii wengine. Yaliyoandikwa ni machache tu. Sababu moja ni kwamba alimtangulia mtu aliye mkubwa zaidi, yaani, Bwana mwenyewe. Inaonekana katika Yohana alivyoeleza kuhusu ubatizo: Yohana alijibu akawaambia wote, Kweli mimi nawabatiza kwa maji; lakini yuaja mtu mwenye nguvu kuliko mimi, ambaye mimi sistahili kuilegeza gidamu ya viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto (m.16). Siku nyingine Yohana alifafanua uhusiano kati yake na Yesu kwa namna hii: Aliye naye bibi arusi ndiye bwana arusi; lakini rafiki yake bwana arusi, yeye anayesimama na kumsikia, aifurahia sana sauti yake bwana arusi. Basi hii furaha yangu imetimia. Yeye hana budi kuzidi, bali mimi kupungua (Yn 3:29-30).

Andiko

siku 28siku 30

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Julai/2022

Soma Biblia Kila Siku Julai/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Julai pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Zakaria na Luka. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/