Soma Biblia Kila Siku Julai/2022Mfano
Luka alianza andiko lake kwa kueleza kuwa nimejitafutia usahihi wa mambo hayo yote tangu mwanzo (1:3). Karibu habari yote ya Lk 1-2 haipo katika injili zile nyingine. Huenda Luka alikuwa ameongea na mama yake Yesu au ndugu zake, k.mf. Yakobo aliyekuwa kiongozi wa usharika mama pale Yerusalemu. Kwa njia hiyo alipata habari kama hii ya leo. Tokea mapema Yesu alijielewa kuwa ni Mwana wa Mungu (taz. m.49). Lakini wazazi wake hawakuelewa sawasawa jambo hili, ingawa malaika alishawajulisha kuwa hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu. … Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake (1:33, 32).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Julai/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Julai pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Zakaria na Luka. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/