Soma Biblia Kila Siku Julai/2022Mfano
Kaisari Augusto alikuwa ni mtawala mkuu wa dola ya Warumi. Kwa hapa Tanzania tungemwita Rais. Na cheo cha yule Kirenio (m.2) ni kama Mkuu wa Mkoa. Utawala wa Warumi ulikuwa ni utawala wenye nguvu na ukubwa ambao ulimwengu ulikuwa haujawahi kuona: Iandikwe orodha ya majina ya watu wote wa ulimwengu (m.1)! Unabii ulitabiri kwamba Kristo atazaliwa katika mji wa Bethlehemu: Wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele (Mik 5:2). Kwa nini Mwana wa Mungu alizaliwa katika hali ya unyonge (m.7,Akamlaza katika hori ya kulia ng'ombe)? Kwa nini hakuzaliwa pale Yerusalemu kwenye ikulu?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Julai/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Julai pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Zakaria na Luka. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/