Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

BibleProject | Kumwamini Mungu katika MatesoMfano

BibleProject | Kumwamini Mungu katika Mateso

SIKU 4 YA 6

Marafiki wa Ayubu wanajibu kuhusu mateso yake kwanza kwa kukaa naye kimya, lakini hatimaye wanaamua kutoa mashtaka ya uongo kuhusu tabia ya Ayubu. Wanachukulia kwamba ikiwa watu ni wazuri na wenye busara, Mungu atawapa mafanikio. Lakini ikiwa watu ni waovu na wapumbavu, Mungu atawaadhibu kwa mateso. Kwa kuwa Ayubu anakabiliwa na janga kuu, marafiki wanachukulia kuwa lazima atakuwa amemkosea Mungu na anaadhibiwa kwa kosa lake. Hata wanafikiria kuhusu dhambi ambazo huenda Ayubu alikuwa amezitenda ili kustahili matokeo mabaya kama hayo. Je, Mungu anawajibu vipi marafiki wa Ayubu?

Jibu la Mungu linakuja mwishoni mwa kitabu anapowahoji marafiki hawa kuhusu Ayubu na jinsi Anavyoendesha ulimwengu. Mitazamo yao kuhusu haki ni finyu sana na hayawezi kuelezea kikamilifu kuhusu uchangamano wa ulimwengu au hekima ya Mungu. Hivyo Mungu Anaghadhabishwa na mashtaka yao dhidi ya Ayubu, lakini Anawahurumia na anawapa fursa ya kupokea neema kupitia maombi ya Ayubu.

Tafakari:
1) Je, kuishi katika ulimwengu ulio jinsi marafiki wa Ayubu walivyochukulia kutakuwaje — ulimwengu ambapo Mungu anaadhibu kila kitendo cha uovu kinachofanywa na watu?
2) Je, unaielezeaje haki ya Mungu?
3) Je, Yesu aliteseka vipi bila kustahili ili kuleta rehema na neema kwa wengine?

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

BibleProject | Kumwamini Mungu katika Mateso

Je, tunawezaje kumwamini Mungu hata pale tunapoteseka bila kustahili? Jiunge nasi katika muongozo huu wa wa siku zita unaotazama simulizi ya Ayubu na ufahamu jinsi kuamini hekima ya Mungu kunaonekaje hata katika vipindi tunapokumbana na magumu.

More

Tungependa kushukuru shirika la BibleProject kwa kutoa mwongozo huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.bibleproject.com/swahili