Ayu 22:1-11
Ayu 22:1-11 SUV
Ndipo huyo Elifazi Mtemani akajibu, na kusema, Je! Yumkini mtu awaye yote kumfaa Mungu? Hakika yeye aliye na hekima hujifaa mwenyewe. Je! Mwenyezi hupata furaha katika wewe kuwa mwenye haki? Au je, ni faida kwake, kwamba wafanya njia zako kuwa timilifu? Je! Ni kwa wewe kumcha yeye anakukemea? Na kuingia hukumuni nawe? Je! Uovu wako si mkuu? Wala maovu yako hayana mwisho. Kwa kuwa umetwaa dhamana kwa nduguyo bure, Na kuwavua nguo zao walio uchi. Hukumpa maji ya kunywa huyo aliyechoka, Nawe umemnyima chakula huyo mwenye njaa. Lakini huyo shujaa, nchi ilikuwa yake; Na huyo mwenye kusifiwa, yeye aliikaa. Umewafukuza wanawake wajane hali ya utupu, Na mikono ya mayatima imevunjwa. Kwa hiyo umezungukwa na mitego, Na hofu ya ghafula yakutaabisha, Au je! Huoni giza, Na maji mengi yanayokufunika?