BibleProject | Kumwamini Mungu katika MatesoMfano
Ayubu, kama vile marafiki wake, anachukulia kuwa ulimwengu uliundwa kwa haki ili haki itunzwe na uovu uadhibiwe. Lakini tofauti na marafiki wake, Ayubu anafahamu kwamba hastahili mateso yake, hivyo anahitimisha kuwa Mungu sio mwenye haki. Je, Mungu anamjibu vipi Ayubu?
Mungu anamjibu Ayubu mwishoni mwa kitabu na anamhoji kuhusu msimamo wake kuwa Yeye sio mwenye haki. Anajitokeza kwa Ayubu katika dhoruba na kumpeleka katika ziara ya mbali ya ulimwengu. Kwenye tufani, Mungu anamuuliza Ayubu maswali magumu kuhusu misingi na uumbaji wa ulimwengu. Je, Ayubu alikuwepo Mungu alipoumba dunia au alipoumba mbingu? Je, Ayubu amewahi kuamuru jua kuchomoza au kudhibiti hali ya hewa? Usemi wa Mungu unaeleza kuwa ulimwengu ni changamani, lakini Mungu pia anafahamu na hutunza vitu vyote. Maelezo yake yanabadili mtazamo wa Ayubu kuwa Mungu sio mwenye haki. Je, Ayubu anajibu vipi?
Haya yote yanamfanya Ayubu kunyenyekea sana. Anakubali kuwa alivuka mipaka, anaomba msamaha kwa kumshtaki Mungu na kurudisha imani yake kwa Mungu. Mungu anamjibu kwa kusema kwamba amenena vyema, hivyo kuwaonyesha wasomaji kwamba tunaweza kuvumilia mateso yetu kupitia maombi ya uaminifu, imani na unyenyekevu.
Tafakari:
1) Je, ni wakati gani ambapo kutambua udhaifu wako kulikufanya unyenyekee?
2) Ayubu anaposema "atajidharau na kutubu" (Ayubu 42:6), hasemi kwamba atajichukia au kuwa hafai mbele ya Mungu. Neno hili la Kiebrania ambalo hutafsiriwa kuwa "kujidharau" pia linaweza kutafsiriwa kuwa "kataa". Ayubu anasema kuwa atakataa kujitegemea mwenyewe na anachagua kuamini maarifa makuu ya Mungu. Je, imekuaje kwako (au kwa wengine) kuamini kwa unyenyekevu kuwa Mungu Anaelewa mateso yetu?
3)Geuza fikira zako kuwa ombi. Mwabudu Mungu kwa uwezo wake na ukuu wa ulimwengu Aliouumba. Kiri uchungu wako na pia kosa lolote la kumkosoa au kumshtaki Mungu. Omba uponyaji wa Mungu na faraja kwako na kwa wote unaojua wanateseka.
Kuhusu Mpango huu
Je, tunawezaje kumwamini Mungu hata pale tunapoteseka bila kustahili? Jiunge nasi katika muongozo huu wa wa siku zita unaotazama simulizi ya Ayubu na ufahamu jinsi kuamini hekima ya Mungu kunaonekaje hata katika vipindi tunapokumbana na magumu.
More
Tungependa kushukuru shirika la BibleProject kwa kutoa mwongozo huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.bibleproject.com/swahili