Soma Biblia Kila Siku Novemba/2022Mfano
Yakobo alimwambia Yusufu, Nitakapolala pamoja na baba zangu, unichukue toka Misri, unizike katika kaburi lao. [Yusufu] akasema, Nitafanya kama ulivyosema. [Yakobo] akanena, Niapie. Naye akamwapia. Israeli akajiinamisha kwenye mchago wa kitanda (m.30-31). Katika Ebr 11:21 tunajifunza kwamba maana ya kujiinamisha hivyo ni kumshukuru Mungu, maana hapo imeandikwa kuwa Yakobo akambariki kila mmoja wa wana wa Yusufu, akaabudu akiegemea kichwa cha fimbo yake. Kwa Israeli ilikuwa jambo muhimu mno kwamba asizikwe Misri, maana Kanaani ndiyo nchi ya ahadi. Na Mungu alimwahidi: Nitakupandisha tena bila shaka (46:4). Yaani, wana wa Israeli walikuwa hawatakaa Misri daima. Iko siku ambapo Mungu atawarudisha Kanaani!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Novemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Novemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mwanzo na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/