Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Novemba/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Novemba/2022

SIKU 20 YA 30

Israeli alikuwa anawabariki wana wake (48:20, Akawabariki siku ile). Ndani ya baraka hiyo kulikuwa na unabii: Kusanyikeni, ili niwaambie yatakayowapata siku za mwisho (m.1). Kabila la Lawi kweli hawakupewa sehemu yao ya nchi ya Kanaani kama makabila mengine. Maana ... yeye Bwana, Mungu wa Israeli, ndiye urithi wao, kama alivyowaambia (Yos 13:32-33). Waligawanyika kama Yakobo alivyosema, Nitawagawa katika Yakobo, nitawatawanya katika Israeli (m.7). Na kabila la Yuda likawa kweli kabila la utawala, mfalme Daudi akiwa wa kwanza. Hata hivyo aliyetimiza kamili ilivyotabiriwa kuwa atakapokuja Yeye, mwenye milki, Ambaye mataifa watamtii (m.8-10) ndiye Mwokozi wetu Yesu Kristo (Masihi). Alitabiriwa kuwa atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake. Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho (Lk 1:30-33).

siku 19siku 21

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Novemba/2022

Soma Biblia Kila Siku Novemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Novemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mwanzo na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/