Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Novemba/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Novemba/2022

SIKU 25 YA 30

Taifa la Israeli lilizungukwa na maadui wengi. Katika somo letu hao wanaangaliwa kuwa maadui wa Bwana, maana Israeli ni watu wake. Mfalme Daudi atawashinda maadui kama inavyoelezwa kuwa, mkono wako utawapata adui zako wote, Mkono wako wa kuume utawapata wanaokuchukia. Utawafanya kuwa kama tanuru ya moto, Wakati wa ghadhabu yako (m.8-9a). Lakini angalia atakavyofanikiwa: Si kwa kulipiza kisasi, bali kwa kumtumainia Bwana (m.7), akimwachia Mungu kuwateketeza maadui (m.9b)! Kwa hiyo ni uwezo wa Bwana unaosifiwa mwisho wa zaburi. Pia waamini wa siku hizi wana maadui. Tukiona maadui wetu ni maadui wa Mungu pia, basi tutumie silaha ya Daudi: Tumwachie Bwana!

siku 24siku 26

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Novemba/2022

Soma Biblia Kila Siku Novemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Novemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mwanzo na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/