Soma Biblia Kila Siku Novemba/2022Mfano
Baada ya Sulemani kumjengea Bwana hekalu, zaburi hii ilitumika kwenye ibada hekaluni. Inueni vichwa vyenu, enyi malango, ... Mfalme wa utukufu apate kuingia (m.7). Ni tendo la upendo Bwana akikubali kukaa katikati ya watu wake. Mtakatifu aliyeumba mbingu na nchi atawezaje kukaa katika hema au jengo la hekalu? Sikia Sulemani anavyoeleza katika 1 Fal 8:27-30: Tazama, mbingu hazikutoshi, wala mbingu za mbingu; sembuse nyumba hii niliyoijenga! Mungu akiwa mwenye utukufu hivyo, atawezaje kukaa mioyoni mwetu? Ndiyo sababu malango yanaambiwa yapanuke, maana Bwana asingestahili kukaa katika unyonge wa namna hii! Tuupokee upendo wake!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Novemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Novemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mwanzo na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/