Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Novemba/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Novemba/2022

SIKU 21 YA 30

Wokovu wako nimeungoja, Ee Bwana (m.18). Yakobo akishamaliza kutabiri habari za Dani, na kabla hajasema la Gadi, hapo ndipo aliponena haya. Ni sala ionyeshayo hamu ya moyo wake. Mungu alimpa kuona mambo mengi mazuri na mabaya yatakayotokea siku zijazo. Kwa hiyo hakuweza kuzuia mdomo wake, akamwomba na kumlilia Bwana kwa sala hii! Katika 1 Pet 1:10-12 imeandikwa kuwa katika habari ya wokovu huu manabii walitafuta-tafuta na kuchunguza-chunguza ambao walitabiri habari za neema itakayowafikia ninyi. Wakatafuta ni wakati upi, na wakati wa namna gani ulioonywa na Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao, ambaye alitangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakaokuwako baada ya hayo. Wakafunuliwa ya kuwa si kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili yenu walihudumu katika mambo hayo, ambayo sasa yamehubiriwa kwenu na wale waliowahubiri ninyi Injili kwa Roho Mtakatifu aliyetumwa kutoka mbinguni. Mambo hayo malaika wanatamani kuyachungulia! - Moyoni una hamu gani?

siku 20siku 22

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Novemba/2022

Soma Biblia Kila Siku Novemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Novemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mwanzo na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/