Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kujiendeleza KibinafsiMfano

Kujiendeleza Kibinafsi

SIKU 1 YA 3

Umuhimu wa Maendeleo.

Ulipokuwa shuleni ungepaswa kufanya mitihani ya mara kwa mara. Mitihani hii humjulisha mwalimu mahali uliposimama kwenye masomo uliyohitaji kujifunza. Ikiwa haukuweza kufaulu mitihani hii, basi mazoezi zaidi na majaribio zaidi yangetolewa.

Mungu pia hutoa mitihani. Mtihani wake unaonyesha mahali tupo kwenye barabara ya maendeleo yetu ya kibinafsi. Mungu hatakuleta kwenye utimilifu wa hatima yako mpaka ajue kwamba unaweza kuisimamia kiroho, kihisia, kimwili na kadhalika.

Ikiwa huwezi kuisimamia, utaipoteza badala ya kuitumia kwa utukufu wake. Ndio maana anazingatia sana maendeleo yetu anapotupeleka kwenye hatima yetu.

Muda na urefu wa kupotoka kwetu maishani mara nyingi inategemea chaguo na ukuaji wetu wa kibinafsi. Mungu anaweza kuwa na mchepuko mfupi uliyopangwa kwa ajili yetu lakini tunaifanya iwe ndefu zaidi kupitia kichwa chetu kigumu, ukaidi, maudhi au kutokomaa na mashaka.

Kwa wale ambao mnafanya mazoezi ya kuujenga mwili, mnajua kuwa misuli yenu inabadilika mara tu baada ya kipindi cha mazoezi ya nguvu? Mchakato unaoitwa kuunganishwa kwa protini hutokea mahali popote kuanzia masaa mawili hadi masaa manne baada ya kufanya mazoezi. Hivi ndivyo misuli inavyokua na nguvu na kubwa. Hata hivyo, ingawa hili hutokea haraka sana baada ya mafunzo ya kutia nguvu, kwa kawaida ni wiki nne hadi sita kabla ya mabadiliko ya misuli yaaonekana na wengine.

Je, umewahi kuanza utaratibu wa kufanya mazoezi kisha ukuacha mara, kwa sababu hukuona matokeo yo yote? Watu wengi hufanya hivyo kwa sababu wanatarajia matokeo haraka zaidi kuliko vile ambavyo matokeo huchukua muda kukua.

Vile vile, watu wengi huacha kufuata njia ya kufikia hatima yao wakati ambapo hawaoni mambo yakipangika haraka jinsi walivyofikiri yanapaswa. Lakini Mungu kwa makusudi anatumia ucheleweshaji na michepuko katika maisha yetu ili kutuendeleza pale anapotupeleka.

Kufikia hatima yako kunahitaji uvumilivu katika mchakato.

Andiko

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Kujiendeleza Kibinafsi

Mara nyingi Mungu hutafuta kutukuza kihisia, kiroho, kimwili na hata katika mahusiano kabla ya kutuinua katika hatima yetu. Tony Evans, ashiriki baadhi ya mawazo muhimu kuhusu umuhimu wa maendeleo ya kibinafsi katika mpango huu wa kusoma.

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/

Mipango inayo husiana