Kujiendeleza KibinafsiMfano
Musa alikuwa kwenye mchepuko kwa muda wa miaka arobaini huku Mungu akimkuza kwa ajili ya hatima yake. Alijua kile ambacho Mungu alitaka afanye. Mungu alimtaka awakomboe watu wake kutoka utumwani. Hata hivyo ilichukua miaka arobaini jangwani kumkuza Musa kuwa mtumishi mnyenyekevu na mwaminifu kama alivyohitajika kuwa, kusudi awe na mawazo, imani na uwezo wa kutekeleza mpango huo.
Ibrahimu alikuwa kwenye mchepuko wa miaka ishirini na mitano. Wakati mmoja, Mungu alikuwa amemwambia mpango wake kwa ajili yake - kwamba angebariki mataifa kupitia Ibrahimu na kulifanya jina lake kuwa kuu. Maono na tangazo kutoka kwa Mungu kwa Ibrahimu yalikuwa ya kweli na wazi. Isingekuwa kawaida kwa Ibrahimu kuamini wakati huo kwamba ingekuwa karibu miongo mitatu kabla ya kushuhudia kuzaliwa kihalisi kwa alichoahidiwa na Mungu. Lakini ndivyo ilikuwa.
Mtume mkuu katika Agano Jipya, Paulo, alifanya safari ya mchepuko kwa miaka mitatu hadi jangwani ambako Mungu alimwondoa katika ukurasa wa mbele wa utamaduni na maisha ili kumtia nguvu, kumfundisha, na kumkuza kwa ajili ya wito wake.
Michepuko mara nyingi ni sehemu ya kawaida ya mpango wa Mungu katika kutuongoza kufikia hatima zetu. Anatumia vipindi hivi katika maisha yetu ili kutukuza kusudi tuweze kutekeleza hatima zetu kwa njia ya kimaadili tunapozifikia.
Mara nyingi Mungu atatupa kuona kidogo tu sehemu ya hatima yetu muda mrefu kabla hatujajitayarisha kuitimiza, kama alivyofanya alipomwambia Ibrahimu kwamba kungekuwa na mchepuko wa miaka 400 huko Misri kabla hawajafika mahali walipoahidiwa (Mwanzo 15:12 16).
Rafiki, usikatishwe tamaa wakati ambapo kuna ucheleweshwaji hadi ukakata tamaa katika kutekeleza kusudi lako. Amini mchakato. Mungu anakuendeleza kwa ajili ya mpango aliokuumba ili uuishi
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Mara nyingi Mungu hutafuta kutukuza kihisia, kiroho, kimwili na hata katika mahusiano kabla ya kutuinua katika hatima yetu. Tony Evans, ashiriki baadhi ya mawazo muhimu kuhusu umuhimu wa maendeleo ya kibinafsi katika mpango huu wa kusoma.
More
Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/