Kujiendeleza KibinafsiMfano
Maendeleo ya kibinafsi sio tukio. Wala si tajriba ambayo ni saizi moja inayofaa wote.Maendeleo huchukua muda, majaribio, kushindwa na kushinda. Mungu anamjua kila mmoja wetu kibinafsi. Anajua kile ambacho kila moja wetu anchohitaji ili kusitawisha na kuimarisha misuli yetu ya kiroho na kunoa ufahamu na hekima yetu ya kiroho. Mara nyingi zaidi, hii inahitaji kuwepo na michepuko katika maisha ili kutupa fursa ya kujifunza, kukua na kuendeleza.
Mungu ana hatima kwa ajili yako. Ana kusudi na mahali anapotaka uishi. Lakini inaweza isitokee kesho. Labda hautafika huko kwa kwenda kwenye mstari ulionyooka. Uvumilivu ni sifa kuu inayohitajika ili kufikia hatima yako.
Hata hivyo, maisha na mchakato wa maendeleo unaweza kuja na masikitiko ya kibinafsi kwa kutamani kwamba ungelikuwa umepiga hatua mbali sana. Kumbuki hili, tumaini halikatishi tamaa. Michepuko inakatisha tamaa, kwa muda mfupi. Lakini tunaporuhusu ilete tumaini - Mungu anaahidi kwamba tumaini halitakatisha tamaa.
Lakini ili wewe ufikie tumaini la kweli katika roho yako – Ni muhimu kukubali michepuko yako.
Kama vile misuli yako haitakua tu kwa kutamani iwe na nguvu. Maumivu kupitia mchakato wa kuimarisha tumaini lako huja kwa michepuko, dhiki, taabu na majaribu.
Nionyeshe mtu aliye na tumaini lisiloweza kushindwa nami nitakuonyesha mtu ambaye amekuwa na sehemu yake ya michepuko. Hii ni kwa sababu matumaini ya kweli ni sifa ya kujifunza. Tumaini la kweli ni kile kiwango cha tumaini ambayo hukaa thabiti licha ya dhoruba na hali ziilizoko. Ni tumaini linalokuwezesha kuendelea kwa imani pekee. Sehemu kubwa ya maendeleo yako ya kibinafsi inalenga kukuza uwezo wako wa kutumaini (kama Ibrahimu) dhidi ya matumaini yote. Kuamini wakati yaonekana kuwa hakuna kitu kinachotendeka. Na kuendelea kutembea kwa imani, licha ya kucheleweshwa.
Unapoendelea kukua kibinafsi, mambo haya yatakuja kwa kawaida zaidi kwako na utashuhudia Mungu akikuingiza katika utimilifu wa hatima yako. Tumia muongozo wa maombi haya kama kichocheo cha maombi yako mwenyewe au jisikie huru kuiomba kwa ukamilifu.
Sala:
Baba wa Mbinguni mwenye upendo, asante kwa zawadi yako ya michepuko. Asante kwa kunipenda kiasi cha kutaka nikue, niwe na maendeleo na kukomaa. Asante kwa kutonipa hatima au ndoto yangu mapema sana, kabla sijawa na uwezo wa kuisimamia - kwa sababu basi, Bwana, naweza kuitumia vibaya, kuipoteza au hata kuiharibu. Mungu - Unajua kilicho bora zaidi. Na Wewe ni Bwana mwenye neema ya kuniendeleza kwa subira ili nifikie mahali pale pa kusudi na hatima yangu. Ninakushukuru mapema kwa yote uliyonayo katika mawazo yako, - katika jina la Kristo, Amina.
Tunatumahi kuwa mpango huu ulikuhimiza. Kwa habari zaidi kuhusu wizara, bofya hapa.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Mara nyingi Mungu hutafuta kutukuza kihisia, kiroho, kimwili na hata katika mahusiano kabla ya kutuinua katika hatima yetu. Tony Evans, ashiriki baadhi ya mawazo muhimu kuhusu umuhimu wa maendeleo ya kibinafsi katika mpango huu wa kusoma.
More
Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/