Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kupokea NenoMfano

Kupokea Neno

SIKU 1 YA 4

Jifunze Neno

“Heri asomaye na wao wayasikiao maneno ya ule unabii, na kuyashika yaliyoandikwa humo; kwa maana wakati umekaribia” (Ufunuo 1:3).

“Heri asomaye,” Yohana asema. Je! Hii inamaanisha kwamba tunapaswa kusoma “aya kwa siku ili kumweka shetani mbali”? Kwa nadra sana. Yeyote anayechukua Biblia na wazo kama hili anaitumia kama hirizi ya bahati nzuri, si kama Neno lenye mamlaka.

Yohana hatuhimizi tuwe na moyo wa kutazama baadhi ya maneno kwenye ukurasa tu. Ana mengi zaidi akilini. Katika Biblia, kusoma kunahusiana na kuelewa kile ambacho Mungu anasema nawe. Wazo si kwamba ungesoma kisha usijue lolote kuhusu yale uliyotoka kusoma sasa hivi, au uliyosoma na useme, “Hapo, nimesoma aya yangu au sura yangu ya leo.”

Wazo la kusoma ni kushika ujumbe wa Mungu kwetu, kujibidiisha zaidi katika kujifunza kwetu "neno la kweli" (2 Timotheo 2:15). Neno la Kigiriki lililotafsiriwa kama “Fanya bidii” katika aya hii inamaanisha kwamba unapofungua Neno, unajitoa kikamilifu kwa hilo. Unakula kama vile unavyokula barua ya upendo. Unaichukulia Biblia kwa uzito.

Kuna mfano mzuri wa hamu aina hii ya Neno katika 2 Timotheo 4:13. Paulo alikuwa mzee, alikuwa gerezani akingoja kufa, na alikuwa mwenye kuona baridi na mpweke. Hapa palikuwa na mtu ambaye alikuwa amekwenda katika mbingu ya tatu, ambaye alikuwa ameona mambo ambayo hakuna mtu mwingine alikuwa ameona (2 Wakorintho 12:14).

Lakini Paulo alitaka nini zaidi ya kitu chochote katika chumba hicho cha gereza chenye unyevunyevu? “Utakapokuja,” alimwandikia Timotheo, “niletee lile joho nililoliacha Troa kwa Karpo, na vile vitabu, hasa vile vya ngozi” (2 Timotheo 4:13).

Karatasi hizi za ngozi zilikuwa nakala za Paulo za Agano la Kale. Kwa maneno mengine, Paulo alikuwa peke yake, mwenye baridi, na asiye na rafiki, lakini alitaka Maandiko. Alijua kwamba Neno la Mungu lingetoa kila kitu kingine chochote ambacho angelihitaji. Paulo alitaka kujifunza Neno hata akiwa gerezani.

Je, unasoma neno kwa urahisi au unajifunza neno kwa ajili ya maarifa ya kina na ufahamu wa Kristo?

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Kupokea Neno

Inaweza kuwa vigumu kujaribu kujitolea kusoma na kujifunza Neno. Katika mpango huu, Tony Evans anafundisha juu ya umuhimu wa kusoma na kulijua Neno ili tuweze kuliruhusu kuleta matokeo katika kila eneo la maisha yetu.

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: Home - The Urban Alternative