Kupokea NenoMfano
Unapoona Neno la Mungu likiwa hai maishani mwako, unapoliona likibubujika kutoka moyoni mwako, na unapomwona Mungu akiliheshimu Neno lake, basi suala la iwapo wewe ni unauwezo wa kukariri Biblia litatoweka. Unapogundua kwamba unaweza kumfukuza shetani akibeba mizigo yake, kwa Neno jinsi Yesu alivyofanya, utajua inafaa kujitahidi kulificha Neno la Mungu moyoni mwako.
Wengi wetu tumekuwa tukimwambia shetani, “Nenda zako; niache.” Lakini haendi popote, kwa sababu sio neno letu ndilo anaogopa. Anaogopa tu Neno la Mungu. Wakristo wengi hawajui kwamba Shetani hawezi kushikamana na Neno. Kwa nini hawezi? Kwa sababu ni nguvu ya Mungu (Warumi 1:16). Yesu alinukuu aya tatu kwa Shetani, naye akaondoka. Mapigo matatu na yuko nje.
Jaribu kutumia Neno dhidi ya ibilisi anapojaribu kuharibu maisha yako, nawe utaona nguvu ya Neno linapotumika katika maisha ya muumini. Unahitaji kusoma Neno; yaani; soma kwa bidii na uikariri.
Tunatumai kuwa mpango huu umekuhimiza. Ili ujue zaid kuhusu huduma ya Tony Evans, bofya hapa.
Kuhusu Mpango huu
Inaweza kuwa vigumu kujaribu kujitolea kusoma na kujifunza Neno. Katika mpango huu, Tony Evans anafundisha juu ya umuhimu wa kusoma na kulijua Neno ili tuweze kuliruhusu kuleta matokeo katika kila eneo la maisha yetu.
More
Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: Home - The Urban Alternative