Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kupokea NenoMfano

Kupokea Neno

SIKU 3 YA 4

Neno haliwezi kuja midomoni mwako na kutoka kinywani mwako hadi liwe kwanza ndani yako, au akilini mwako. Katika Mithali 22:17 18, tunasoma ushauri huu:

“Tega sikio lako, uyasikie maneno ya wenye hekima, ukaelekeza akili yako katika maarifa yangu; kwa maana itapendeza ukiyaweka ndani yako, yakawe tayari midomoni mwako.

Kisha mwandishi anasema, “Nimekufundisha leo... Je! sikukuandikia mambo yaliyo bora ya mashauri na maarifa? (Mithali 22:19 – 20).

Anasema, "Niliandika kile unachohitaji, lakini unapaswa kukiweka ndani yako." Ikiwa utashirikiana na Roho kwa kufanya kazi ya kukariri Maandiko, yeye anaweza kuweka akilini mwako kile kinachohitaji kutoka kinywani mwako unapokabili hali ngumu na matatizo.

Unaweza kuwa unasema, “Tony, hunijui mimi. Sina uwezo mzuri wa kukariri mambo.” Najua watu ambao wanaweza kukumbuka kila mchezaji kwenye kila timu ya NFL na chuo gani walichochezea kabla ya kuwa wachezaji wa kulipwa. Na ninawajua watu ambao wanaweza kunukuu mistari kutoka kwa kila aina ya sinema. Ikiwa unaweza kukariri mambo haya madogo, unaweza kukariri maneno ambayo huletea watu uzima,

Kwa wengi wetu, mpango halisi ni kwamba hatujisikii kukariri maandiko ya Biblia. Hebu chukulia kwamba utapewa dola elfu kumi kwa kila aya unayokariri. Ungekuwa bingwa wa kukariri Biblia ulimwenguni. Hizo dola elfu kumi zingekupa chembe chembe za ubongo ambazo hukujua ulikuwa nazo hapo awali. Kwa nini? Tuzo hilo lingestahili jitihada hiyo.

Nabii Ezekieli anasema kwamba Mungu alipomwambia ale gombo lenye Neno lake kwa Israeli, lilikuwa tamu kama asali katika kinywa cha Ezekieli (Ezekieli 3:1 – 3). Ladha yake ilikuwa ni nzuri. Thamani ya jitihada yake ilistahili. Utajua tu iwapo kitu ni cha thamani kutokana na jitihada unapoweka jitahada ya kujua.

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Kupokea Neno

Inaweza kuwa vigumu kujaribu kujitolea kusoma na kujifunza Neno. Katika mpango huu, Tony Evans anafundisha juu ya umuhimu wa kusoma na kulijua Neno ili tuweze kuliruhusu kuleta matokeo katika kila eneo la maisha yetu.

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: Home - The Urban Alternative