Pumziko Kwa WaliochokaMfano
Yesu anawaita wale waliochoka na kulemewa na mizigo waje kwake, wapate pumziko.
Katika Injili ya Mathayo, Yesu aliwashutumu waandishi na Mafarisayo kwa sababu wao
“hufunga mizigo mizito na kuwatwika watu mabegani mwao, lakini wao wenyewe hawataki kuisogeza hata kwa kidole” (Mathayo 23:4).
Tofauti na orodha ya sheria, matakwa, na kushika sheria ambazo waandishi na Mafarisayo walitaka watu wazishike ili washiriki kikamilifu katika imani ya Israeli, Yesu aliwaita umati waliochoka na kulemewa na mizigo waje kwake.
Wito wa Yesu ni mwito kwa wale wote waliokuwa wamechoshwa na kukata tamaa katika juhudi zao wenyewe za kuingia katika uhusiano naye. Uhusiano huu unakuja bila sharti au mazungumzo ya kimkataba. Ni zawadi ya neema, kipawa cha ukarimu kinachotolewa kwa wote wanaomwendea, na Yesu anaahidi kwamba wote wanaoitikia watapewa pumziko (Mathayo 11:28).
Kwa nini kuja kwa Yesu kunatoa tumaini la “kupumzika” kwa “waliochoka na kulemewa na mizigo?”
Kuhusu Mpango huu
Mpango huu wa kusoma na Dk. Tony Evans utakupa mtazamo wa kina zaidi wa amri tatu zilizotolewa na Yesu ambazo zitakusaidia kuingia katika msimu wa mapumziko maishani mwako.
More
Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/