Pumziko Kwa WaliochokaMfano
Je, ni kwa jinsi gani tunajifunza kuinyenyekea nira rahisi ya Yesu kama Bwana wetu?
Sharti la tatu ambalo Yesu alitoa katika kifungu hiki lilikuwa hili:
“Jifunzeni kwangu, kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtapata raha nafsini mwenu” (Mathayo 11:29).
Tunaingia katika shule ya Yesu ya nira rahisi na mzigo mwepesi kwa kuishi maisha kama alivyoishi. Tunapojifunza kuhusu maisha yake katika Maandiko na kujibu kwa utiifu wa maombi, tutajifunza kufuata amri yake:
“…Mtu ye yote akitaka kunifuata, ni lazima ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate. Kwa maana yeyote anayetaka kuokoa maisha yake atayapoteza; lakini mtu atakayeipoteza nafsi yake kwa ajili yangu ataiona” (Mathayo 16:24 – 25).
Kwa kifupi, twajifunza kutoka kwa Yesu, kwa kujitolea kufanyika kuwa wanafunzi wake. Huketi kwenye miguu yake huku tukiiga mwenendo wa maisha yake hadi hapo ambapo maisha yake yatakuwa maisha yetu kabisa.
Sitaki ufikiri kwamba kuja kwa Yesu, kuchukua nira yake, na kujifunza kutoka kwake inamaanisha kwamba tutaondolewa kimiujiza miujiza kutoka kwenye mizigo na mateso yetu. Hata hivyo inamaanisha, kwamba mzigo utaonekana kuwa mwepesi tunapopata kwamba tumefungwa nira kwa Yule ambaye aliyekuwa na nguvu za kutosha kubeba uzito wa dhambi zetu zote msalabani.
Je, umejitolea kuwa mfuasi wa Yesu—sio tu mtu ambaye amepokea toleo lake la wokovu, lakini mtu ambaye anatafuta kwa bidii kuiga mwenendo wake wa kuishi katika maisha yako mwenyewe?
Tunatumai kuwa mpango huu umekuhimiza. Ili ujue zaid kuhusu huduma ya Tony Evans, bofya hapa.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Mpango huu wa kusoma na Dk. Tony Evans utakupa mtazamo wa kina zaidi wa amri tatu zilizotolewa na Yesu ambazo zitakusaidia kuingia katika msimu wa mapumziko maishani mwako.
More
Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/