Soma Biblia Kila Siku/ FEBRUARI 2023Mfano
Binadamu tunaishi kwa kusaidiana na kushauriana. Hapa duniani kuna washauri wa aina mbalimbali. Mfalme Rehoboamu alipokutana na jambo gumu aliwaendea washauri wa aina mbili. Wazee walimpa ushauri wa kumsaidia, lakini vijana wenzake wakampa ushauri wa kumpotosha. Yeye akachukua ushauri ambao ulimpotosha. Ukipewa ushauri, omba Mungu akupe hekima ya kuchambua na kuchukua ulio mzuri. Ukikubali kuwa mtumishi wa watu ... basi watakuwa watumishi wako daima (m.7). Kila kiongozi azingatie hili.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku/Februari 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Warumi na 1 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/