Soma Biblia Kila Siku/ FEBRUARI 2023Mfano
Ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu (m.18). Kabla Paulo hajaendelea kufundisha zaidi juu ya Injili anaonyesha jinsi Mataifa (1:18-32) na Wayahudi (2:1-3:20) wanavyopotea na kuhukumiwa na ghadhabu ya Mungu. Kuna makosa mawili ya msingi yanayomtenganisha Mmataifa na Mungu: 1. "Uasi", yaani kutokumwamini na kumtukuza Mungu. Kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza … (m.21-23). 2. "Uovu", yaani kufanya yasiyo haki. Hawa ni waipingao kweli kwa uovu (m.18). Je, uko chini ya ghadhabu ya Mungu?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku/Februari 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Warumi na 1 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/