Soma Biblia Kila Siku/ FEBRUARI 2023Mfano
Wewe ujisifuye katika torati, wamvunjia Mungu heshima kwa kuiasi torati? (m.23). Paulo anawakemea Wayahudi. Mungu amewapa mwanga wa pekee katika neno lake (torati), mwanga ambao Mataifa hawana. Kutokana na mwanga huo wao wamepewa wajibu na nafasi ya kuwa viongozi wa vipofu, mwanga wa walio gizani, wakufunzi wa wajinga, walimu wa watoto wachanga, wenye namna ya maarifa na ya kweli katika torati (m.17-20). Lakini mwanga huu usipowafanya waishi katika imani ya kweli, hautawasaidia lolote, kwa maana kutahiriwa kwafaa kama ukiwa mtendaji wa sheria, lakini ukiwa mvunjaji wa sheria kutahiriwa kwako kumekuwa kutokutahiriwa (m.25). Mioyo yao iko mbali na Mungu. Ni wanafiki. Wana alama ya kuwa Wayahudi, lakini wamemwasi Mungu. Yeye ni Myahudi aliye Myahudi kwa ndani (m.29). Swali: Je, sisi tu Wakristo kweli kwa ndani?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku/Februari 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Warumi na 1 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/