Soma Biblia Kila Siku/ FEBRUARI 2023Mfano
Lo! Haya ni maneno mazuri mno! Mungu amelifungua lango kubwa na pana la kufika kwake Mbinguni kwa kila binadamu! Maana hakuna tofauti; kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu (m.22-24). Hata ukijiona kwamba ni mwenye dhambi sana na umepotea, mlango huu uko wazi kwako. Njoo kwa Yesu kama ulivyo leo hii. Piga magoti! Fungua moyo wako, umwambie mambo yote! Na umshukuru kwa wokovu wake!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku/Februari 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Warumi na 1 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/