Soma Biblia Kila Siku/ FEBRUARI 2023Mfano
Akili haikubali wokovu wa bure namna hii! Je, Ibrahimu hakufanya tendo lolote ili apewe uheri huu? Huenda alikuwa ametahiriwa kwanza na halafu imani yake ikahesabiwa kuwa ni haki (m.9-10)? Hapana, hapana! Neema ni neema, haina madai yoyote. Kutahiriwa kwa Ibrahimu kulifuata baadaye kama alama ya kuthibitisha kuwa alikwisha hesabiwa haki kwa imani (m.11)! Aliyetahiriwa na asiyetahiriwa wana hali hii moja: Wote wanahesabiwa haki bure kwa kuamini neema ya Mungu iliyofunuliwa katika Yesu Kristo!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku/Februari 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Warumi na 1 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/