Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku/ FEBRUARI 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku/ FEBRUARI 2023

SIKU 9 YA 28

Paulo anaonyesha jinsi kila binadamu anavyoonekana machoni pa Mungu. Huenda machoni pa watu wengine na hata machoni petu wenyewe tunaonekana watu wema. Lakini kwa Mungu sivyo. Kumcha Mungu hakupo machoni pao (m.18). Maana Mungu anadai ukamilifu! Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote (Mt 22:37). Ukamilifu huu hajauona kwa mtu yeyote (m.10-12). Kwa hiyo njia ya kuokolewa ni kwa neema ya Mungu tu. Kwa kupewa sheria Wayahudi walisaidiwa sana kutambua hali hiyo ya watu wote. Kwa tafakari zaidi rudia m.19-20, uzingatie maana yake, Paulo anaposisitiza hivi, Twajua ya kuwa mambo yote inenayo torati huyanena kwa hao walio chini ya torati, ili kila kinywa kifumbwe, na ulimwengu wote uwe chini ya hukumu ya Mungu; kwa sababu hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki mbele zake kwa matendo ya sheria; kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria.

siku 8siku 10

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku/ FEBRUARI 2023

Soma Biblia Kila Siku/Februari 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Warumi na 1 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/