Soma Biblia Kila Siku/ Machi 2023Mfano
Angalia sababu mbili za Paulo kuweza kuandika twajua uteule wenu (m.4): 1. Injili si maneno tu, bali Roho Mtakatifu hufanya kazi ndani yake. Kwa hiyo ina nguvu ... na uthibitifu mwingi (m.5, Injili yetu haikuwafikia katika maneno tu, bali na katika nguvu, na katika Roho Mtakatifu, na uthibitifu mwingi). 2. Wathesalonike waliipokea Injili kwa furaha ya imani (m.6, Mkawa wafuasi wetu na wa Bwana, mkiisha kulipokea neno katika dhiki nyingi, pamoja na furaha ya Roho Mtakatifu). Kwa sababu ya nguvu yake, Injili huwageuza wale waipokeao, yaani a) wanaojutia maovu yao, wakiacha kilichochukua nafasi ya Mungu maishani mwao (m.9, Jinsi mlivyomgeukia Mungu mkaziacha sanamu, ili kumtumikia Mungu aliye hai, wa kweli), na b) wanaomtegemea Yesu, wakimfuata (m.6, Mkawa wafuasi wetu na wa Bwana), kumtumikia (m.9, Mkaziacha sanamu, ili kumtumikia Mungu aliye hai, wa kweli), na kutazamia kuja kwake (m.10, Na kumngojea Mwanawe kutoka mbinguni ... Yesu, mwenye kutuokoa na ghadhabu itakayokuja). Utumie sababu hizo mbili, ukijibu swala hili, Je, umeteuliwa na Mungu?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku/Machi 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wathesalonike na Yohana. Karibu kujiunga na mpango huu bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/