Soma Biblia Kila Siku/ Machi 2023Mfano
Wayahudi walitumia viatu vilivyokuwa wazi. Kwa hiyo wakiwa safarini, miguu yao ilichafuka kwa urahisi. Walikuwa na desturi ya kutawadha (kunawa) miguu wakijiandaa kula. Hawakukalia viti wakati wa kula bali walikaa chini kwenye sakafu. Kwa hiyo ilikuwa muhimu zaidi kuwa na miguu safi. Yesu akijua kwamba hapo karibuni atarudi kwa Baba, alitenda tendo hili la pekee ili kuwaonyesha kwamba aliwapenda upeo (m.1; m.3-5 inathibitisha hiyo kwa jinsi Yesu alivyokuwa tayari kuwatumikia). Pia aliwapa wanafunzi wake kielelezo kwa kuwatadha miguu. Yesu mwenyewe anawaambia katika m.12-16. Heri ninyi mkiyatenda (m.17)!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku/Machi 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wathesalonike na Yohana. Karibu kujiunga na mpango huu bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/