Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku/ Machi 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku/ Machi 2023

SIKU 22 YA 31

Shetani alimwingia Yuda (m.27). Lakini kuanguka kwake hakukuanza siku hiyo. Kuanzia huko nyuma alitunza mfuko wao (m.29). Lakini alianza kuiba fedha hizo kwa kuwa ni mwivi, naye ndiye aliyeshika mfuko, akavichukua vilivyotiwa humo (12:6). Upendo wake kwa Yesu ukapoa. Mwisho akaamua kuwasaidia Wayahudi kumkamata Yesu ili kupata fedha nyingi. Hilo ni onyo kwetu! Mara tukiona dhambi yoyote ikitaka kuingia katika mawazo yetu tukiri mbele ya Yesu! Maana dhambi ikishapata nafasi huzidi kupata nguvu na mwisho hutuangusha! Kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa. Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti. Ndugu zangu wapenzi, msidanganyike (Yak 1:14-16).

siku 21siku 23

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku/ Machi 2023

Soma Biblia Kila Siku/Machi 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wathesalonike na Yohana. Karibu kujiunga na mpango huu bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/