Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku/ Machi 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku/ Machi 2023

SIKU 27 YA 31

Taifa la Israeli walikuwa mzabibu wa Mungu, lakini wakageuka wakawa mzabibu mwitu usiofaa. Katika Yeremia 2:21 tunasoma, Nami nalikuwa nimekupanda, mzabibu mwema sana, mbegu nzuri kabisa; umegeukaje, basi, kuwa mche usiofaa wa mzabibu-mwitu machoni pangu? Sasa Yesu anajitangaza kwamba yeye ndiye Mzabibu wa kweli. Matawi ni wale wakaao ndani yake (m.5, Ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake). Wakaao ndani yake ni hao ambao neno lake hukaa ndani yao. Inaonekana wazi tukilinganisha m.5 na 7: Ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana - Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa (ling m.3, Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia). Je, wewe ni mmoja wao? Tambua kwamba Yesu siye shina tu, bali ni mzabibu wote, yaani shina pamoja na matawi! Hii inaonyesha umoja mkubwa ulioko kati ya Yesu na walio wake (m.5, Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote)! Yeye ndiye anatufanya tuzae matunda mema!

Andiko

siku 26siku 28

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku/ Machi 2023

Soma Biblia Kila Siku/Machi 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wathesalonike na Yohana. Karibu kujiunga na mpango huu bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/