Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku/ Machi 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku/ Machi 2023

SIKU 30 YA 31

Yesu huwatia moyo wanafunzi kwa kuwaambia kwamba akisharudi kwa Baba yake atawapelekea Msaidizi. Jina lingine ni Roho wa kweli au Roho Mtakatifu (Yn 14:25; 15:26 na 16:5-7). Kazi yake itakuwa ni kuwaokoa wanadamu (m.8-11) na kuwatia wanafunzi wa Yesu katika kweli yote (m.13, Atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote). Zaidi sana atamshuhudia na kumtukuza Yesu kwao (15:26 na 16:14). Ikiwa YESU anashuhudiwa na kutukuzwa maishani mwako ni dalili moja muhimu kuwa Roho wa kweli hufanya kazi ndani yako! Yohana ameeleza hili kwa kusema, Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani. Katika hili mwamjua Roho wa Mungu; kila roho ikiriyo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatokana na Mungu. Na kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani (1 Yoh 4:1-3).

siku 29siku 31

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku/ Machi 2023

Soma Biblia Kila Siku/Machi 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wathesalonike na Yohana. Karibu kujiunga na mpango huu bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/