Soma Biblia Kila Siku/ Machi 2023Mfano
Tukitaka kupata kitu kwa mtu mkubwa, mara nyingi inasaidia tukimpitia mtu ambaye yupo karibu na huyo mkubwa na wakati huohuo yupo karibu nasi. Leo Yesu anatufundisha kwamba ndivyo ilivyo kwa Mungu. Yesu Kristo ni Mpatanishi wetu, naye anatukaribisha kwenda pamoja naye kwa Baba. Zingatia Yesu anavyoeleza katika m.12-14, Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba. Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya. Yesu ni mwombezi wetu kwa Mungu. Tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki, naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote (1 Yoh 2:1-2). Kwa hiyo omba kwa jina la Yesu, yaani, omba ukimtegemea yeye! Mfuasi wa Yesu afanyaye hivyo huambiwa na Yesu, Kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya (m.12).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku/Machi 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wathesalonike na Yohana. Karibu kujiunga na mpango huu bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/