Siku Sita Za Majina Ya MunguMfano
SIKU YA 1: EL EMUNAH – MUNGU MWAMINIFU
Tunapenda kufikiria kuwa sisi ni watu waaminifu. Tunaingia kazini kwa wakati (vizuri, kwa kawaida) na kufanya kazi yetu kwa bidii. Tunatenga wakati wa kuwa na familia na marafiki. Tunahusika katika kanisa letu na kujiandikisha kuhudumu kwa kamati zilizopo na fursa za kujitolea panapo hitajika. Lakini hata tujitahidi kadiri gani kuwa waaminifu, sisi si wakamilifu. Bila shaka, tutakosa mkutano au tukose kuhudhuria mchezo wa soka wa mtoto au kusahau kazi hiyo ya kujitolea.
Kwa sababu hatuwezi kuwa watu waaminifu siku zote, inatia moyo kujua kwamba tunamtumikia Mungu mwaminifu. Jina lake El Emunah linamaanisha “Mungu Mwaminifu,” na anaweza kutegemewa siku zote kujitokeza, kukunja mikono ya vazi lake na kuanza kufanya kazi maishani mwetu. Daima hutimiza ahadi zake? Ndiyo. Daima husikia maombi yetu? Ndiyo. Daima hubaki kuwa nasi? Ndiyo.
Mambo hutokea katika maisha yetu ambayo yanatuzuia tusiwe waaminifu kabisa kwa wengine. Kwa sababu sisi ni binadamu, tunajaribiwa kufanya maamuzi kulingana na nia yetu ya kujihifadhi, ubinafsi na uchoyo. Kwa urahisi kabisa, hatuwezi kuwa wakamilifu kila wakati. Lakini tusipojitokeza, Mungu hujitokeza. Na Yeye hutuongoza kwa upole kurudi kwa kazi aliyo nayo hasa kwa ajili yetu kufanya—kazi ya kuwa waaminifu na kujitokeza kwa ajili ya wengine. Tunapogeukia ukamilifu wake katika nyakati zetu za kutokamilika, uaminifu wake hutubadilisha.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Kutoka kwa majina mengi aliyo nayo Mungu, Yeye ametufunulia vipengele vya tabia yake na asili yake. Zaidi ya majina haya ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, Biblia inaonyesha majina zaidi ya 80 tofauti ya Mungu. Hapa kuna majina sita na maana zake ili kumsaidia muumini kumkaribia Mungu Mmoja wa Kweli. Hii ni dondoo kutoka kwa kitabu cha Uzoefu wa Nguvu ya Majina ya Mungu: Ibada itoayo Maisha ya Kuishi na Dk. Tony Evans.
More
Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/