Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Siku Sita Za Majina Ya MunguMfano

Siku Sita Za Majina Ya Mungu

SIKU 5 YA 6

SIKU YA 5: ELOHE TSADEKI – MUNGU WA HAKI YANGU

Daima tunatafuta jambo kubwa linalofuata. Siri ya kujipanga. Ufunguo wa kupata umbo nzuri. Mpango wa uhakika wa uhifadhi na kuwa dhabiti kifedha. Tunasoma vitabu, tunasikiliza podikasti na kujiandikisha kwa seminaa. Na ingawa kujipanga, utimamu wa mwili na usalama wa kifedha ni shughuli zinazofaa, tunahitaji kuhakikisha kuwa hatukosi picha kuu tunapotafuta jambo kuu linalofuata.

Jambo kuu la maisha ni kumfuata Mungu, kuwa kama yeye na kuishi maisha yetu kwa ajili yake. Na kuwa kama Mungu inamaanisha kukua katika wema na haki. Kutoka kwa Bwana hutiririka rehema, neema, uwezo na nguvu—sifa zote tunazohitaji katika maisha yetu na katika ulimwengu wetu. Mungu hutupa yote tunayohitaji kupitia Neno lake na Roho wake ili tuishi katika furaha tele. Tunapochagua matamanio yake badala ya yetu na kujitahidi kuwa kama Yeye zaidi, yeye hutuongoza na kutuelekeza.

Kufuata mpango wa Mungu kunaweza kuwa na changamoto zaidi kuliko kushikamana na hatua sita rahisi za kuwa na mwili timamu au njia kumi za kuondoa mkusanyiko wa ovyo wa vitu nyumbani kwako. Lakini pia ina faida zaidi, tunapomgeukia Mungu na kukabidhi maisha yetu kwake, yeye hutusamehe na kutupa zawadi kwa huruma yake. Anasaidia kurekebisha mahusiano yetu yaliyovunjika na kuijaza mioyo yetu haki, neema na amani. Matunda mazuri huja kwa kumfuata Mungu na kuruhusu haki yake kuongoza hatua zetu.

siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

Siku Sita Za Majina Ya Mungu

Kutoka kwa majina mengi aliyo nayo Mungu, Yeye ametufunulia vipengele vya tabia yake na asili yake. Zaidi ya majina haya ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, Biblia inaonyesha majina zaidi ya 80 tofauti ya Mungu. Hapa kuna majina sita na maana zake ili kumsaidia muumini kumkaribia Mungu Mmoja wa Kweli. Hii ni dondoo kutoka kwa kitabu cha Uzoefu wa Nguvu ya Majina ya Mungu: Ibada itoayo Maisha ya Kuishi na Dk. Tony Evans.

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/