Siku Sita Za Majina Ya MunguMfano
SIKU YA 2: ELOHE CHASEDDI – MUNGU WA REHEMA
Maisha huwa hayatuhakikishii nafasi za pili. Kuna nyakati ambapo maamuzi yetu mabaya—maneno makali yaliyosemwa kwa rafiki, makosa tuliyofanya kazini, maamuzi ya maisha yasiyofaa—yanatugharimu. Tunapoteza urafiki. Tumefukuzwa kutoka kwenye kazi yetu. Afya zetu zinadhoofika. Hata kama tuna mabadiliko ya moyo, hakuna uhakika kwamba kila kitu kitakuwa sawa.
Ingawa hivyo, rehema ya Mungu, inatupa nafasi ya pili baada ya nafasi ya pili. Elohe Chaseddi — Mungu wa rehema — hutunyeshea msamaha na hutuogesha kwa fadhili zenye upendo. Yeye ni mwaminifu kila wakati. Daima mwenye rehema. Daima mwenye huruma. Ikiwa tunampenda na kumwomba msamaha, Yeye hutupatia. Kila mara.
Kwa sababu Yeye ni Mungu wa rehema, tunaweza kuishi bila woga. Daima tuna njia ya kupata amani ya akili na moyo ambayo Yeye hutoa bure na kwa wingi. Anaahidi kuwa nasi daima na kutuvusha katika kila hali ya taabu na kila msimu mgumu. Hata wakati makosa yanafanywa na sisi wenyewe, Yeye yuko tayari daima kutoa msamaha kwa moyo uliotubu.
Badala ya kuhangaikia jana, Mungu anataka tuzingatie leo. Je, tunawezaje kumtumikia leo? Je, ana mipango gani ili tuweze kuitimiza leo? Je, tunawezaje kumshirikisha na wengine leo? Huo ndio uzuri wa rehema—nafasi ya pili, kutazama mbele, kwa kuzingatia wakati ujao alio nao kwetu.
Kuhusu Mpango huu
Kutoka kwa majina mengi aliyo nayo Mungu, Yeye ametufunulia vipengele vya tabia yake na asili yake. Zaidi ya majina haya ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, Biblia inaonyesha majina zaidi ya 80 tofauti ya Mungu. Hapa kuna majina sita na maana zake ili kumsaidia muumini kumkaribia Mungu Mmoja wa Kweli. Hii ni dondoo kutoka kwa kitabu cha Uzoefu wa Nguvu ya Majina ya Mungu: Ibada itoayo Maisha ya Kuishi na Dk. Tony Evans.
More
Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/