Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kusudi La KirohoMfano

Kusudi La Kiroho

SIKU 2 YA 3

Utambuzi wa kina zaidi wa utambulisho wetu wa kiroho hutusaidia kutambua kusudi letu la kiroho.

Changamoto ya Yeremia kwa Waisraeli waliohamishwa haikuwa kutafuta kusudi lao bali, kama watu wateule wa Mungu, wamtafute Mungu kwanza katikati ya hali zao. Hata hivyo, ilikuwa ni katika kumfuata na kumtafuta Mungu kwa mioyo yao yote (Yeremia 29:13) ambapo makusudi na mipango ya Mungu kwa ajili ya watu wake hufanyika wazi kwao:

“Nami nitawarudishieni fanaka zenu na kuwakusanya kutoka mataifa yote na mahali pote nilipowafukuzia. Nitawarudisheni mahali ambapo niliwatoa, nikawapeleka uhamishoni.” (Yeremia 29:14).

Unaweza kuona mtindo kama huo ukifanya kazi katika wito wa Sauli na Barnaba kuwa wamishonari katika kitabu cha Matendo Ya Mitume:

"Wale (kanisa la Antiokia) walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, 'Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia' (Matendo Ya Mitume 13:2).

Ilikuwa ni pale tu kanisa la Antiokia lilipomtafuta Mungu na kujifunza zaidi kutoka moyoni mwake ndipo Roho Mtakatifu alitoa upambanuzi kuhusu wito wa Sauli na Barnaba kwa utume ambao Mungu alikuwa ameuweka kwa ajili ya kanisa lake.

Wengi wetu katika maisha hukosa mwelekeo kwa sababu tunafuata kusudi ambalo halifuati utaratibu wa tabia yake Mungu na kile alichotuumba tuwe. Kama vile mzazi anavyomsahihisha mtoto anayetumia vibaya chombo cha jikoni, Mungu anawaambia wengi wetu kuhusu mwelekeo wa maisha yetu, “hilo halijatengenezwa kwa ajili ya kazi hil o!”

Je, unasikiliza Mungu anapokuelekeza kwenye njia ya kusudi lako?

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Kusudi La Kiroho

Tukiangalia maagizo ambayo Yeremia alitoa kwa watu waliohamishiwa Babeli, tunaweza kujifunza kweli zinazohusu kutafuta kusudi letu, na hilo tulilo kusudiwa kuwa kwa ajili ya Kristo. Mpango huu wa kusoma na Dk. Tony Evans utaelezea tatu kati ya kweli hizo.

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/