Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023

SIKU 17 YA 30

Ni vigumu kung’amua uwepo wa wachonganishi na waleta shari katikati yetu, lakini Mungu anasema wapo, “Kwako wamo wanaowasingizia wengine ili wauawe. … Watu wako wanatenda ufisadi” (Eze 22:9). Watu wa namna hii wapo nyumbani na kanisani mwetu pia. Wanajipendekeza ili wapate umaarufu na kupendwa kwa njia ya uongo. Usaliti huletwa kwa unafiki. Uongo na uchonganishi huleta chuki katika jamii. Sifa kuu ya Kristo ni kuleta amani na upendo. Jenga nia ya kuwatakia watu heri na amani.

siku 16siku 18

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa septemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Warumi na Methali. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/