Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 09/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 09/2024

SIKU 12 YA 30

Mambo yote yaliyotabiriwa kuhusu Yesu, hata aina ya kaburi alimozikwa, yalitimia, na yameendelea kudhihirika hata leo. Kwa mfano habari ya Isa 53:9 ilitimia katika kifo chake kilicholeta wokovu:Wakamfanyia kaburi pamoja na wabaya; Na pamoja na matajiri katika kufa kwake; Ingawa hakutenda jeuri, Wala hapakuwa na hila kinywani mwake. Ijapokuwa Yesu alidharauliwa na kudhalilishwa, heshima na ufalme wake uliendelea, na bado unaendelea kudhihirika kwa watu wote. Hakuna nguvu wala mamlaka itakayoweza kuuzuia au kuufunika ukuu wa Yesu. Yeye ataadhimishwa katika maeneo yote ya maisha yetu. Kwa sababu hiyo astahili kuwa Bwana wetu sisi sote.

siku 11siku 13

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 09/2024

Soma Biblia Kila Siku 09/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Tisa pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz

Mipangilio yanayo husiana