Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 09/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 09/2024

SIKU 14 YA 30

Baada ya kufufuka, Yesu alijidhihirisha kwa wengi, kama Paulo anavyodhihirisha wazi katika 1 Kor 15:5-8. Kwanza Kristoalimtokea Kefa; tena na wale Thenashara;baadaye aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano pamoja; katika hao wengi wanaishi hata sasa, ila baadhi yao wamelala;baadaye akamtokea Yakobo; tena na mitume wote;na mwisho wa watu wote, alinitokea mimi, kama ni mtu aliyezaliwa si kwa wakati wake.Hata leo Yesu anaendelea kujidhihirisha kuwa yu hai kwa njia ya kuendelea kuokoa na kuleta maisha mapya kwa wote wanaomwamini. Waliomwua walitumia fedha na kutunga uongo ili kujaribu kuuzima ukweli. Hata kuna watu wanaodanganyika wakiamini kuwa mwili wa Yesu uliibwa na maiti yake kufichwa. Lakini hakuna mashaka! Bwana Yesu alikufa na akafufuka siku ya tatu, kama yanenavyo Maandiko. Na ufalme wake unaendelea kuenea duniani pote.

siku 13siku 15

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 09/2024

Soma Biblia Kila Siku 09/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Tisa pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz