Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 09/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 09/2024

SIKU 16 YA 30

Yehoshafari wa Yuda alikuwa rafiki wa nyumba ya Ahabu, mfalme wa Israeli. Matokeo yake yakawa mabaya. Alifanya mwana wake kumwoa Athalia, binti Ahabu, naye binti huyu alileta dini ya ubaali nchini Yuda. Yehoramu, mumewe, aliathiriwa, akafuata njia mbaya ya Ahabu na Yezebeli:Akaiendea njia ya wafalme wa Israeli kama walivyofanya nyumba ya Ahabu; kwa kuwa alikuwa amemwoa binti Ahabu; akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana(m.18). Ilikuwa kwa sababu ya ile ahadi tu ambayo Mungu alimpa Daudi, kwamba ufalme wa Yuda haukuangamia:Bwana hakupenda kuiharibu Yuda, kwa ajili ya Daudi mtumishi wake, kama alivyomwahidia akasema, kuwa atampa taa, yeye na wazao wake siku zote(m.19). Lakini Yuda kupoteza umiliki wa Edomu waliofaulu kupiga jeshi la Yuda. Basi, tafakari wema na ukali wa Mungu.

siku 15siku 17

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 09/2024

Soma Biblia Kila Siku 09/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Tisa pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz

Mipangilio yanayo husiana