Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 09/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 09/2024

SIKU 25 YA 30

Yoashi anafuata mapenzi ya Bwana muda wote kuhani Yehoyada anapomshauri. Anaamuru sadaka za nadhiri na za kujitolea zitumike kwa kukarabati hekalu. Lakini kazi hii haiendi sawa. Je, makuhani hawakuwa waaminifu au walikosa bidii tu? Hatujui. Lakini hata baada ya kutawala miaka 23 bila mafanikio Yoashi hajakata tamaa, bali anaweka utaratibu mwingine ili kuhakikisha fedha inayokusanywa inakwenda kwenye mfuko wa ujenzi. Tujifunze kwake ikiwa usimamizi wa fedha ya kanisa una changamoto.

siku 24siku 26

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 09/2024

Soma Biblia Kila Siku 09/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Tisa pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz

Mipangilio yanayo husiana