Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 09/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 09/2024

SIKU 29 YA 30

Wapo watu wanaojivunia utajiri na nguvu zao na kuwanyanyasa wengine. Wote, yaani maskini kwa tajiri, ni kazi ya Mungu. Mwimbaji wa zaburi hii anatukumbusha kuwa maisha ya tajiri na maskini ni sawa, kwani wote wanakufa. Tajiri hawezi kumpa Mungu fedha ili azuie kifo chake. Kwa fedha watu hawawezi kununua haki ya kuendelea kuishi. Hata mtu angekuwa na fedha kiasi gani, kifo ni lazima. Kinachotakiwa kwa tajiri na maskini ni kumtegemea Mungu na ukombozi wake, wakiamini kama mwimbaji wa zaburi hii katika m.15:Mungu atanikomboa nafsi yangu, Atanitoa mkononi mwa kuzimu, maana atanikaribisha. Kwake Mungu kuna uzima wa milele.

siku 28siku 30

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 09/2024

Soma Biblia Kila Siku 09/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Tisa pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz

Mipangilio yanayo husiana