Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 09/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 09/2024

SIKU 26 YA 30

Pamoja na kubadilisha utaratibu wa kukusanya fedha, waliajiriwa watendakazi waaminifu ili watunze hesabu ya malipo na kufanya kazi vizuri. Utaratibu huo ulihakikisha pia fedha za kutosha kwa ajili ya makuhani.Fedha ya matoleo ya kosa, na fedha ya matoleo ya dhambi, haikuletwa nyumbani mwa Bwana; hiyo ilikuwa ya makuhani wenyewe(m.16). Ila sasa alitokea adui wa nje ya nchi, yaani mfalme Hazaeli wa Shamu. Yoashi alizuia kutekwa kwa Yerusalemu kwa kumpa Hazaeli hazina zote za hekalu na ikulu, lakini watu wa Yoashi hawakuridhika na utawala wake. Hata tunasoma katika 2 Nya 24:25 kwambawatumishi wake mwenyewe wakamfanyia fitina kwa ajili ya damu ya mwana wa Yehoyada kuhani, wakamwua kitandani pake, akafa; wakamzika mjini mwa Daudi, lakini hawakumzika katika makaburi ya wafalme. Tafakari mwisho wa mwenendo wake.

siku 25siku 27

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 09/2024

Soma Biblia Kila Siku 09/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Tisa pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz

Mipangilio yanayo husiana