Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Msingi Wa Mungu UsiotikisikaMfano

Msingi Wa Mungu Usiotikisika

SIKU 1 YA 4

Mungu asiyetikisika ndiye Kimbilio Langu

Zaburi 46. Tamko la kuabudu kutoka kwa taifa la Israeli, Zaburi ya kusifu nguvu za Mungu na uwepo wake kwa watu wake wakati wote. Zaburi 46 inaonyesha muujiza wa ukombozi wa Mungu kwa watu wake na hali yake ya kutokubadilika katika mazingira ya kukatisha tamaa sana.

Maneno ya Zaburi hii ni ukumbusho mzuri kwamba Mungu hatuachi wakati mazingira yakiwa magumu. Yupo hapo hapo pamoja nasi, na habadiliki. Mungu wetu ambaye yupo wakati wote yeye haathiriki na changamoto za dunia hii, nguvu zake na uwepo wake havitaweza kubadilishwa kwa kuhamisha maadili, mawazo tofauti au dunia isiyo imara.

Wakati mazingira ya maisha yanatishia kutulemea, tunaweza kupata kimbilio na pumziko katika Mungu wetu apatikanaye mda wote na asiyebadilika. Tunaweza kushikilia ufahamu kwamba Mungu yuko pamoja nasi na kwa usalama wa kutambua kwamba nguvu za Mungu hazitishwi na majanga asilia (Zaburi 46:2-3) wala vita (Zaburi 46:8-9).

Mungu amehakikisha uwezo wake wa kutuangalia na kututunza sisi, Tunapokuwa wazi kwake, yeye siyo mzito wa kuona au kutambua, yeye yuko karibu na anapatikana. Tunaweza kuamini kwamba yeye ni Mungu pamoja nasi naye atabakia yule yule. Katikati ya vurugu na maangamizo, yeye hutoa mahali salama, amani, na ulinzi.

Tunaweza kupata kimbilio katika Bwana mweza yote, kimbilio letu na nguvu, msaada unaopatikana tele wakati wa mateso.

Kutafakari:

Soma vifungu vya Zaburi 46 mara kadhaa. Vifungu hivi inaweza kuwa umevizoea. Visome taratibu na kwa makusudi.

Unapofikiria kuhusu maisha yako na dunia unamoishi, ina maana gani kwako kuthibitisha kwamba Mungu ni kimbilio, nguvu yako, yuko pamoja nawe naye atakusaidia unapokabiliana na matatizo?

Hii hukufanya ujisikie namna gani?

Unahitaji kukumbuka nini kutoka kwenye kutafakari kwako Zaburi 46 leo? Chukua muda kiasi kuandika au kurekodi mawazo yako.

Maombi:

Baba wa Mbinguni,

Katikati ya kutokuwa na uhakika, tunapata hakikisho katika uwepo wako usiobadilika. Wewe ndiye kimbilio na nguvu zetu, msaada utakaopatikana tele wakati wa mateso. Twaomba tupate faraja katika uhakika wa uwepo wako na maarifa ya pendo lako lisiloshindwa.

Amina.

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Msingi Wa Mungu Usiotikisika

Tunapofikiria hali ya dunia tunayoishi ndani yake, mahali vita na migogoro vinaonekana kutawala kila kituo cha habari, majanga ya asili yanawakumba watu duniani na mahali ambapo mahusiano yaliyo vunjika ni ya kawaida ndani ya jamii, tunatazama Zaburi 46, inayotupa ujasiri kwamba Mungu ndiye msingi usiotikisika katika mazingira yoyote. Tunabadilika, mazingira yetu yanabadilika, lakini Mungu wetu habadiliki.

More

Tungependa kumshukuru The Salvation Army International kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://salvationarmy.org

Mipangilio yanayo husiana