Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Msingi Wa Mungu UsiotikisikaMfano

Msingi Wa Mungu Usiotikisika

SIKU 2 YA 4

Mungu Asiyetikisika Hunipa mimi Ujasiri

‘Kwa hiyo, hatutaogopa, ingawa dunia inatoa nafasi na milima inaanguka ndani ya moyo wa bahari’.

Sisi hatutaogopa.

Haya madai ya ujasiri. Madai ambayo sio kila mara ni rahisi kuwa dhahiri katika maisha yetu, hasa tunapoona machafuko, kutokuwa na uhakika, hatari na mateso katika dunia yetu, katika familia zetu na katika jamii zetu.

Hofu ni mwitikio wa asili wa binadamu, na ni majibu yanayoweza kutusukuma kwenye matendo yasiyofikirika au kutuzuia sisi kutembea kabisa. Hofu ya usalama wetu, hofu ya matokeo, hofu ya yasiyojulikana. Hofu inaweza kulemaza.

Kuna wakati ambao mambo yanayotokea kutuzunguka, mazingira katika maisha yetu wenyewe au hadithi tunazoziona katika majarida huonekana kuwa hayawezekani kukabiliwa. Tunaweza tukajikuta tunauliza:

Mungu yuko wapi katika yote haya?

Kwanini Mungu hayazuii haya kutokea?

Nini kitatokea kwangu na kwa wale ninaowapenda?

Kuna nyakati hatutaelewa kile kinachoendelea kutuzunguka sisi. Tunaweza kuuliza maswali haya lakini tunaweza tusipate majibu. Kuna nyakati kutoogopa, na kuwa jasiri vinaonekana kuwa sio rahisi. Lakini wema wa Mungu hautegemei tunavyojisikia.

Hizi ndizo nyakati ambazo lazima tuwaegemee wengine wanaotusaidia, wale wanaosimama kwa mshikamano na sisi. Tunaposikia sauti zinazoaminika, sauti za wale tunaowafahamu na kuwapenda, zikitangaza wema wa Mungu na uaminifu wake, tunaweza kupata tumaini na nguvu katika kuwaamini wao na upendo wao. Tukijizungushia mambo yanayotukumbusha Mungu ni nani na ahadi zake kwetu, tunaweza kupata ujasiri wa kuendelea kuamini.

Hatutakiwi kuwa na hofu. Kwanini? Kwasababu Mungu ndiye kimbilio letu, nguvu yetu, msaada wetu wakati wa mateso. Na yeye yuko pamoja nasi.

Kutafakari:

Je, kuna mambo maishani mwako mda huu, ndani ya maisha ya watu unaowapenda, au katika dunia yanayofanya iwe vigumu kwako kusema, ‘Sitaogopa’?

Ni zipi hizo sauti za kuaminika zinazotangaza wema na ahadi za Mungu katika maisha yako?

Je, wewe unaweza kuwa sauti inayoaminika kwa mtu mwingine? / Anayehitaji wewe uwe sauti inayoaminika kwake mda huu?

Maombi:

Mpendwa Bwana,

Wakati kila kitu kunizunguka kinaponichanganya na kuniogopesha, asante kwamba wewe ndiye Mungu asiyetikisika anayenifahamu mimi na anayeelewa ninavyojisikia. Wewe ndiye anayenipa ujasiri nikabiliane na hofu zangu na anayenisaidia kunifanya niendelee, hata wakati maisha yanapoonekana kuwa magumu. Napumzika kwa kufahamu kwamba wewe upo pamoja nami.

Amina.

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Msingi Wa Mungu Usiotikisika

Tunapofikiria hali ya dunia tunayoishi ndani yake, mahali vita na migogoro vinaonekana kutawala kila kituo cha habari, majanga ya asili yanawakumba watu duniani na mahali ambapo mahusiano yaliyo vunjika ni ya kawaida ndani ya jamii, tunatazama Zaburi 46, inayotupa ujasiri kwamba Mungu ndiye msingi usiotikisika katika mazingira yoyote. Tunabadilika, mazingira yetu yanabadilika, lakini Mungu wetu habadiliki.

More

Tungependa kumshukuru The Salvation Army International kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://salvationarmy.org

Mipangilio yanayo husiana