Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Msingi Wa Mungu UsiotikisikaMfano

Msingi Wa Mungu Usiotikisika

SIKU 4 YA 4

Ujasiri wangu uko katika Mungu asiyetikisika

Zaburi 46 inaishia na ukumbusho kwamba tunapomzingatia Mungu, tutaona uwezo wake katika kila hali na katika kila hatua ya maisha yetu. Inatukumbusha kwamba Mungu ni Mungu, na Mungu yuko pamoja nasi. Tumehakikishiwa uwepo wa Mungu hata katika zile nyakati ambazo mazingira yetu binafsi au matukio ya dunia yanachukua sehemu kubwa ya maisha yetu na nguvu mpaka tunaona vigumu kutambua kwamba Mungu yupo pamoja nasi.

Kama wanafunzi katika njia ya kuelekea Emau (Luka 24:13-35) panaweza pakawepo nyakati ambazo hatutambui kwamba Mungu yuko pamoja nasi au kwamba uwepo wa Mungu, nguvu zake vinatosha kwa mahitaji yetu. Lakini Mungu yupo na hata kama mazingira yetu hayabadiliki, uwepo wake, na nguvu zake vinabakia kuwa ni toshelevu.

Maisha yetu na uzoefu wa dunia ni wa tofauti sana na mwandishi wa zaburi. Hata hivyo, tunaweza kuchagua kudai ujasiri unaokuja kutokana na kujua kwamba Mungu ni Mungu, naye ataendelea kuwa Mungu.

Licha ya hofu yetu, tunapokumbuka kazi za Mungu katika historia na katika maisha yetu wenyewe, tunaweza kuwa na uhakika kwamba Mungu ndiye msingi usiotikisika kwa hali yoyote.

Kutafakari:

Arch R. Wiggins aliandika maneno haya: ‘… nikiwa peke yangu barabarani, nikiwa nimefinywa na mzigo wangu, Yesu mwenyewe alinikaribia na akatembea nami’.

Je, huko ‘kutembea na’ kunafananaje kwako?

Maombi:

Mpendwa Bwana,

Ujasiri wangu uko katika wewe na enzi yako kuu iliyo juu ya vitu vyote. Kati ya changamoto za maisha na kutokuwa na uhakika, nisaidie macho yangu yasibanduke kwako, Mungu asiyetikisika. Katika uwepo wako, napata pumziko nami nadai hili kwangu leo.

Asante Yesu.

Amina.

siku 3

Kuhusu Mpango huu

Msingi Wa Mungu Usiotikisika

Tunapofikiria hali ya dunia tunayoishi ndani yake, mahali vita na migogoro vinaonekana kutawala kila kituo cha habari, majanga ya asili yanawakumba watu duniani na mahali ambapo mahusiano yaliyo vunjika ni ya kawaida ndani ya jamii, tunatazama Zaburi 46, inayotupa ujasiri kwamba Mungu ndiye msingi usiotikisika katika mazingira yoyote. Tunabadilika, mazingira yetu yanabadilika, lakini Mungu wetu habadiliki.

More

Tungependa kumshukuru The Salvation Army International kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://salvationarmy.org