Soma Biblia Kila Siku 12/2024Mfano
Mataifa yote wanaalikwa kumsifu Bwana kwa shangwe, kwa sababu Mungu aliye mfalme mwenye mamlaka ameshuka kuwaokoa watu wake. Baada ya ushindi wa vita, Mungu amerejea mbinguni na kuketi katika kiti chake cha enzi. Sifa hizi pia zinamhusu Yesu. Yesu aliacha utukufu wake akaja duniani kutuokoa, kisha akapaa mbinguni, na sasa anamiliki mataifa yote. Watu wote wapo chini yake, hivyo ametukuka.Mungu awamiliki mataifa, Mungu ameketi katika kiti chake kitakatifu. Wakuu wa watu wamekusanyika, Wawe watu wa Mungu wa Ibrahimu. Maana ngao za dunia zina Mungu, Ametukuka sana(m.8-9). Paulo anatueleza kuwa Yesu aliacha utukufu huo, akaja kwetu kama mwanadamu ili atuokoe.Mwanzo [Yesu]alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba. Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba(Flp 2:6-11).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 12/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi na mbili pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na Waebrania. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz