Soma Biblia Kila Siku 12/2024Mfano
Kurudi kwa Bwana Yesu kutatanguliwa na ishara ya wazi. Na hatimaye, atakapokuja, vilio vya huzuni vya waliombeza vitaijaza anga, wakati hoihoi za furaha zitasikika kwa waliomwamini. Ni siku ya ajabu wateule watakapokuwa wanakusanywa mbele ya Mfalme Yesu kwa mashangilio makuu. Bwana atuonya tusome matukio ya ulimwenguni. Yatatuandaa na kutuhakikishia kwamba Bwana Yesu yu karibu mlangoni. Nayo yatutosha kujiandaa kumlaki badala ya kudadisi tarehe ya tukio hilo ambayo Mungu ameiweka sirini mwake.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 12/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi na mbili pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na Waebrania. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz