1
Mhubiri 8:15
Neno: Maandiko Matakatifu 2024
Kwa hiyo mimi ninasifu kufurahia maisha, kwa sababu hakuna kitu bora zaidi kwa mwanadamu chini ya jua kuliko kula, kunywa na kufurahi. Kisha furaha itafuatana naye kazini mwake siku zote za maisha yake ambazo amepewa na Mungu chini ya jua.
Linganisha
Chunguza Mhubiri 8:15
2
Mhubiri 8:12
Ingawa mtu mwovu hufanya maovu mia moja na akaendelea kuishi maisha marefu, najua kwamba itakuwa bora zaidi kwa watu wanaomwogopa Mungu, wamchao Mungu.
Chunguza Mhubiri 8:12
3
Mhubiri 8:6
Kwa maana kuna wakati mwafaka na utaratibu wa kila jambo, ingawa huzuni ya mwanadamu huwa nzito juu yake.
Chunguza Mhubiri 8:6
4
Mhubiri 8:8
Hakuna mwanadamu awezaye kushikilia roho yake asife, wala hakuna mwenye uwezo juu ya siku ya kufa kwake. Kama vile hakuna yeyote arudishwaye nyuma wakati wa vita, kadhalika uovu hautawaweka huru wale wautendao.
Chunguza Mhubiri 8:8
5
Mhubiri 8:11
Wakati hukumu juu ya tendo ovu haitekelezwi upesi, mioyo ya watu hujaa mipango ya kutenda maovu.
Chunguza Mhubiri 8:11
6
Mhubiri 8:14
Kuna kitu kingine ambacho ni ubatili kinachofanyika duniani: Watu waadilifu kupata yale yanayowastahili waovu, nao waovu kupata yale yanayowastahili waadilifu. Hili nalo pia, nasema ni ubatili.
Chunguza Mhubiri 8:14
7
Mhubiri 8:7
Kwa vile hakuna mtu ajuaye siku zijazo, ni nani awezaye kumwambia linalokuja?
Chunguza Mhubiri 8:7
Nyumbani
Bibilia
Mipango
Video